Asema ataka kuniona nadeka..
Asema moyo hutulia akiona nacheka..
Asema kwangu yeye mateka..
Asema hakuna mwengine anayemtataka..
Asema mi na yeye hatuto fikia talaka..
Asema kwangu ametia waraka..
Asema kupitia yote hatoniacha..
Asema ataka tuzae mapacha..
Asema popote naendapo atanifuata..
Asema kwangu ashafika,kubwaga mchezo wa karata..
Asema nimo moyoni..
Asema tupendane hadi ukingoni..
Asema uzuri wangu kamgeuza mpagawa..
Asema twende mkahawani tunywe kahawa..
Asema japo kuna kulia..
Asema kwa pamoja tutavumilia..
Asema kwangu ametua..
Asema ashapata kwake shambani ua..
Asema kwa wote amewapitia..
Asema kwangu mimi ameshikilia..
Asema nina weupe wa mnato..
Asema hao wengine hawanacho..
Asema ameonja utamu..
Asema habanduki ni vigamu..
Asema namtia hamu..
Asema tukajivinjari ya mahaba lamu..
Asema anipenda.
Asema ‘ahenda,usije kunitenga..umenishika moyo ganzi-vaa pete nikupe mapenzi.’